By Doreen Soita

Kufikia sasa wizara ya elimu haijapokea maelezo kuwahusu wanafunzu zaidi ya laki moja ambao walifanya mtihani wa kcpe mwaka jana huku sasa wizara ikisema itaimarisha juhudi kuhakikisha kila aliyefanya mtihani huo atajiunga na shule ya secondari.
Wakati huo huo wanafunzi 2,299 waliofanya mtihani huo wamejiunga na taasisi za kiufundi jambo ambalo wazori amina mohammed anasema halifai

Akizindua rasmi kampeni ya kitaifa ya wiki moja kuwatafuta wanafunzi 133, 574 ambao walifanya mtihani wa KCPE na hawajafika katika shule za upili walizoitwa, waziri wa elimu Amina Mohammed ameonekana kugadhabishwa na hatua ya baadhi ya wanafunzi kujiunga na taasisi za kiufundi. Kampeni hiyo inalenga kaunti ambazo zimewasajili wanafunzi chini ya asilimia 70 Nairobi ikiwa mojawapo ya kaunti hizo.

Aidha waziri Amina amewaagiza machifu kwa ushirikiano na maafisa wa elimu kuwatafuta wanafunzi hao ili kufanikisha mpango wa kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa KCPE anaingia shule ya upili.

Kulingana na waziri baadhi ya changamoto ambazo zimezuia kufaulu kwa mradi huo ni pamoja na mimba za mapema, ndoa za mapema, utovu wa usalama , mila na tamaduni pamoja na umasikini hasa katika maeneo kame.
Kwa sasa wanafunzi asilimia 87 wamejiunga na kidato cha kwanza kaunti ya Muranga ikiongoza kwa usajili wa wanafunzi asilimia 97.

Leave a comment