Mapenzi, matamu kama asali
Mapenzi, Amani ya afadhali
Mapenzi, sumu tapeli
Mapenzi, kitu kipi kama mapenzi!

Mapenzi, Siri ya roho kuu
Mapenzi, kila kukicha sikukuu
mapenzi, takuonyesha makuu
mapenzi,kitu kipi kama mapenzi!

Mapenzi, takufanya uje ua
mapenzi, takupa lako ua
mapenzi, si Siri yako jua
Mapenzi,kitu kipi kama mapenzi!

Mapenzi, yasojua chozi
Mapenzi, chozi liso kohozi
Mapenzi, ni yako jahazi
Mapenzi, kitu kipi kama mapenzi!

Mapenzi, kilio cha furaha
Mapenzi, pigo lenye Raha
Mapenzi, majonzi ya karaha
Mapenzi,kitu kipi kama mapenzi!

Mapenzi, februari yamepata
Mapenzi, yapo Kwa kila sakata
Mapenzi, hivi sasa ni matata
Mapenzi,kitu kipi kama mapenzi!

-watare. B

One thought on “Ushairi. Mapenzi !

Leave a comment